Uhandisi wa Maumbile
Swala la uhandisi wa maumbile ni swala linaloleta utata sana, kutoka kwa uhandisi wa mimea hadi ule wa wanyama na binadamu. Bila shaka kuna faida zinanazoambatana na huu uhandisi, kwa mfano nchi Amerikani hivi leo wanavuna chakula kinachokidhi mahitaji yao wenyewe na ya nchi nyingi duniani. Vile vile, katika upande wa binadamu huu uhandisi umesaidia kurekebisha magonjwa fulani yaliodhaniwa kutokuwa na tiba hapo awali. Hata hivyo, kuna wengi ambao wana wasiwasi kuhusu madhara ya uhandisi kama huu. Kwa mfano watu wengi wametazama kwamba miongo kadha iliyopita watu barani Afrika walikuwa hawapati magonjwa kama kansa, lakini leo kuna watu wengi ambao wanafariki kutokona na kansa.Kweli kunao wanaodhani kuwa mojawapo ya sababu ambazo zimechangia jambo jili ni uhandisi wa chakula. Hata hivyo wengine wamesema kuwa japo kuna ripoti zinazoonyesha kwamaba vyakula hivi havina madhara, havijakuwepo kwa urefu unaotosha kuhakikisha havina madhara yanoyojitokeza baada ya muda mrefu sana, au katika vizazi vinayofuata. Hili ni swali lilohitaji kujadiliwa na kufanyiwa utafiti zaidi.
No recent comments found.